Sadio Mane amejumuishwa kwenye kikosi cha Senegal kitakachoshiriki Kombe la Dunia nchini Qatar licha ya kusumbuliwa na majeraha siku ya Jumanne. Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 30 alilazimika kutoka nje katika kipindi cha kwanza cha ushindi wa 6-1 wa Bayern Munich dhidi ya Werder Bremen.